Social Icons

Pages

Featured Posts

Blogger news

Thursday, August 22, 2013

Jokate a.k.a Kidoti atoboa siri za kuzimikiwa na wanaume wengi….Diamond atajwa!


Mrembo anayefanya vizuri katika mambo mengi sana nchini Jokate Mwegelo amezungumza na kutaja Mambo manne yanayomfanya apendwe sana na wanaume wengi hapa nchini.
1. Kujiamini
Hii ndi sababu kubwa ya kwanza aliyoitaja jokate. Ansema hamna kitu kinachowavutia watu, hasa wananume kama kujiamini. Mwanaume anapenda msichana anayejiamini. Zaidi ya yote hamna kitu kinachosema kuwa “I’m sexy” Zaidi ya mwanamke anayejiamini
2. Kujitegemea
Hii ni kama sababu ya kwanza hapo juu,  Jokate anasema hamna kitu kinachowaboa wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe unapenda kutafuta vya kwako basi jua atakupenda sana
3. Kupendeza
Jokate anasema ni muhimu kwa wadada kuvaa nguo nzuri ambazo zitakupendeza kulingana na mwili wako hasa hasa nguo zenye rangi ya kuonekana.
4. Tabasamu
Tabasamu kila saa kwani tabasamu linakufanya unaonekana mzuri Zaidi.


Wachunguzi wa mambo wamesema kuwa sababu hizi ndio pia zilichangia Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini Diamond platnumz kumpenda mwanadada huyu kwani sifa hizi hazipo kwa wadada wengi wa mjini

Friday, October 12, 2012

Uzinduzi wa Kidoti











Kidoti ambayo ni chapa halisi ya Kitanzania imezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.

Chapa ya Kidoti imeundwa katika taswira yake mwenyewe Jokate.

Sifa zake alizohakikisha zinaonekana kupitia Kidoti ni pamoja na akili, ujasiri, dhamira, yenye kuthubutu lakini pia yenye bashasha zote za kike.

Kidoti haitaishia katika mavazi na mitindo tu.

Kidoti ni harakati na mwanzo wa chapa ya mitindo-maisha yenye nia kuu ya kuwezesha kizazi change,” aliongeza Jokate.

Nywele sanisi za Kidoti ambazo zimezinduliwa leo katika soko ni zenye ubora wa hali ya juu zikiwa zimejaribiwa na wateja wake watarajiwa wenyewe.

Mtiririko mzima wa ubunifu na uzalishaji wa bidhaa hizi ulisimamiwa na kuongozwa na Jokate ambapo kila nywele zimejaribiwa na kukidhi matakwa ya kudumu, kuweza kutumiwa tena na tena, uzito pamoja na msokotano.

Nywele hizi zinakuja katika mitindo na urefu mbalimbali ambayo imebeba sifa za chapa hii zikiwa na mawimbo nyororo kwa ajili ya wanawake wanaopenda kupendeza bila kufilisi mifuko yao.

Pamoja na ubora wake wa hali ya juu, nywele hizi zinaendana kabisa na nia ya Kidoti ya kuvuruga na kuleta maana mpya katika tasnia ya mitindo kwa ubunifu wa kuweza kutengeneza mitindo mingi kutumia nywele moja na sifa hii inawasilishwa kwa soko walengwa kibunifu kupitia kasha za bidhaa hizi ambazo zimesheheni picha za Jokate mwenyewe akionyesha mitindo mbalimbali kwa ajili ya kila nywele. Sifa hii ya kipekee pia inawasilishwa kupitia maneno “nywele moja staili kibao!” yaliyochapishwa katika kila kasha.

Nywele za Kidoti zitapatikana kwa bei nafuu kupitia mawakala mbalimbali wa jumla na rejareja jijini kuanzia leo na zitauzwa kwa kati ya Sh. 9,500 na 12,000.

Mawakala hawa ni pamoja na maduka ya jumla na rejareja Kariakoo, saluni mbalimbali jijini na mtandao wa mawakala mikoani utakaokuwa na bidhaa zetu kuanzia wiki ijayo.

Nguo za Kidoti zitatambulishwa rasmi katika soko mwakani (2013) zikifuatiwa na vifuasi vya urembo pamoja na vipodozi.

Harakati ya Kidoti inaendeshwa na timu ya vijana wabunifu pamoja na kwamba shughuli za Kidoti zinaendeshwa kutoka Dar es Salaam, chapa hii ni ya kiulimwengu zaidi.

Chapa ya Kidoti ilianzishwa mwaka 2011 na Bi. Jokate Mwegelo ambaye ni mmoja wa watu mashuhuri nchini, kwa nia ya kubadilisha mtazamo mzima wa tasnia ya mitindo. Chapa hii itasheheni bidhaa mbalimbali zikiwemo nywele za sanisi ambazo zimezinduliwa leo pamoja na chapa. Bidhaa nyinginezo ni pamoja na nguo, vifuasi vya urembo pamoja na vipodozi.

Kidoti ni chapa yenye uwezo wa kubadilisha jinsi tunavyoichukulia tasnia ya mitindo hivi sasa.
 

Sample text

Sample Text

Sample Text